Tangazo la Zabuni Halmshauri ya Mji wa Mafinga

HALMASHAURI YA MJI WA MAFINGA

TANGAZO LA ZABUNI

(Barua zote ziandikwe kupitia kwa Mkurugenzi wa Mji)

TANGAZO LA MWALIKO WA MAKAMPUNI BINAFSI YA UPANGAJI NA UPIMAJI (URASIMISHAJI) KUFANYA URASIMISHAJI SHIRIKISHI WA VIWANJA TAKRIBANI 19,000 KATIKA HALMASHAURI YA MJI WA MAFINGA.

Halmashauri ya Mji wa Mafinga imepanga kufanya upangaji na upimaji shirikishi(Urasimishaji) wa viwanja takribani 19,000 kwa mwaka wa fedha 2019/2020 kwa kutumia bajeti inayotokana na michango ya wananchi ambao wameendeleza ujenzi katika maeneo mbalimbali ambayo yapo katika eneo la kiutawala la Halmashauri ya Mji wa Mafinga.

1. Halmashauri inakusudia kuwa Mapato ya fedha zitakazotokana na wananchi zitatumika kulipia malipo halali ya mikataba ambayo itatolewa kutokana na mwaliko wa kazi hii inayohusu upangaji na upimaji shirikishi.

2. Makampuni binafsi yenye sifa na uzoefu yanayotambuliwa na Wizara ya Ardhi nyumba na maendeleo na Makazi na yaliyosajiliwa na Bodi za kitaaluma za upangaji na upimaji yanakaribishwa kuleta maombi yao kwaajili ya kufanya kazi tajwa hapo juu kwa mitaa iliyoainishwa  kwenye jedwali  hapa chini:-

Jedwali: 1 MAENEO YANAYOTARAJIWA KUPANGWA NA KUPIMWA

4. Maombi yote yawe na nakala halisi (Original) moja na nakala mbili zinazofanana na yatumwe kwa Mkurugenzi, Halmashauri ya Mji wa Mafinga, S.L.P 76 Mafinga

5. Mwisho wa kuwasilisha maombi haya ni tarehe 19/12/2019 siku ya Alhamisi saa 4:00 Asubuhi. Maombi yatakayoletwa baada ya muda na tarehe tajwa hayatapokelewa.

6. Tangazo hili pia linapatikana katika website ya Halmashauri ya Mji wa Mafinga www.mafingatc.co.tz

                                                         SAADA S. MWARUKA

                                                              MKURUGENZI

                         HALMASHAURI YA MJI WA MAFINGA